Ticker

10/recent/ticker-posts

MSANII MAMA ABDUL AWACHARUKIA WALIOSUSIA KITABU CHA KANUMBA

Muigizaji mkongwe nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’.
Na Deogratius Mongela /UWAZI
MUIGIZAJI mkongwe nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’ amewacharukia mastaa wa filamu Bongo kwa kususia kujitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha Kanumba.
Akizungumza na Uwazi, Mama Abdul aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuisha kwa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Landmark, Ubungo Riverside ambapo alisikitishwa kutokana na marehemu kuwa mchango mkubwa katika tasnia ya filamu.
“Wasanii wetu ni wanafiki, wanapata wapi jeuri ya kumtenga Mama Kanumba wakati kwenye msiba walikuwa wote? Au tuseme wameona kwenye uzinduzi hakuna namna ya kupiga dili kama walivyozoea watawakosa watu wa kuwauzia sura.”Mama Kanumba( wa tatu kulia) akiwa na wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha Kanumba.
“Wamenikera, halafu wakimuona Mama Kanumba wanajifanya kumsalimia kinafiki. Bongo hakuna kama Kanumba waache kujishauwa,” alisema Mama Abdul.