Ticker

10/recent/ticker-posts

USIKU WA KHANGA ZA KALE 2013”, LEO NOVEMBA 8 -SERENA HOTEL

leotena_d9d54.jpg
HAPATOSHI NDANI YA SERENA HOTEL LEO NOVEMBA 8
MAMA ASHA BILAL NDANI NA MASTAA KIBAO
Na Andrew Chale
"LEO ndio Leo, lile Onesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013, 'Extra Vaa Khanga Party' ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa ya Novemba 8.
Katika onesho hilo, jioni ya leo, Mke wa wa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Asha Bilal anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kusindikiza usiku huo ambao pia utapambwa na mastaa mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, ikiwemo burudani murua kutoka kwa bendi ya Mashauzi Classic.
Mkurugenzi wa Fabak Fashion, Asia Idarous, ambao ndio waandaji wa maonyesho hayo, amesema tofauti na maonyesho mengine yaliyotangulia, Kanga ya Kale ya mwaka huu ina ladha tofauti kidogo ilikuwapa radha wadau wake..
"Licha ya kuonyesha matoleo mapya na mitindo ya kanga pia kuonyesha yale ya zamani ili kuleta vionjo zaidi kwa wavaaji wa sasa, tunakusudia kutoa darasa kuhusiana na thamani ya kanga japo kwa muda mfupi tu", alisema.
Na kuongeza kuwa, usiku huo vazi la khanga ndilo litakuwa maalumu kwa wadau watakaohudhuria sambamba na kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
Kiingilio katika onyesho hilo ni sh 30,000 na viti maalumu itakuwa ni sh 50,000 ambako tiketi zinaendelea kuuzwa Fabak Fashions Mikocheni na Gift Shop Serena Hotel pamoja na mlangoni hapo hapo Serena hotel.
Aidha, usiku wa Khanga za Kale umedhaminiwa na Redd's, CXC, Clouds FM, Vayle Spring, Magic FM, Eye View, Amina Design, Kabile, Voice of America, Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times FM, Michuzi Media Group, Event Light na Miss Tanzania, New Africatv.com, Kajuna blog,Vijimambo blog na wengineo kibao.
Maonyesho ya Kanga za kale nchini yanafanyika kwa mara ya tano tangu pale yalipoanzishwa rasmi mwake mwaka 2008
Mwisho

Post a Comment

0 Comments