Mamlaka ya udhibiti na ununuzi wa
umma(PPRA)wameanza mafunzo maalum ya kutoa taarifa za manunuzi kwa njia ya mtandao kwa maafisa ugavi na asasi zinazofanya
ununuzi kwa kutumia fedha za umma yaani Procurement Management Information System(PMIS).
Baadhi wa wasiriki wa mafunzo hayo ya siku nne yanayoendeshwa na mamlaka ya udhibiti ya ununuzi wa umma PPRA
Mafunzo hayo ambayo yalifunguliwa na kaimu afisa mtendaji mkuu wa PPRA,Mhandisi Dkt.Laurent Shirima yalianza jana tarehe 12 /11
katika hoteli ya Naura Springs iliyopo jijini Arusha na yanatarajiwa kukamilika tarehe
15 mwezi huu ambapo washiriki zaidi ya 100 toka idara mabalimbali za serikali watatunukiwa
vyeti ya kuhitimu mafunzo hayo yenye
lengo la kuboresha mfumo wa kutumia
teknolojia katika kutoa ripoti mbalimbali za manunuzi.
0 Comments