Mpishi Maarufu Nchini Bw.Justin Mwabuki,''Chef Mwabuki'' maarufu kama "msanii wa nyama." ameshinda tuzo ya mpishi bora wa mwaka kwa mwaka 2023/2024 tuzo zilizotolewa wiki iliyopita jijini Dar es salaam..Mwabuki ambaye ni Muasisi na Mmiliki wa mgahawa maarufu Jijini Dar es Salaam unaofahamika kwa jina la On Point Kitchen & BBQ, uliopo Mbezi Beach Africana jirani na kituo cha mabasi cha Rafia anatambulika kwa ustadi wake wa upishi, hasa katika kuandaa nyama safi na za bei nafuu, zinazosifika kwa matoleo ya ladha kama vile chipsi za viungo na michuzi ya pilipili (pilipili).
Katika ukiurasa wake wa mtandao wa Instagram wa @onpointkitchenstz, ambapo anashiriki maudhui kuhusu kazi na falsafa yake, aliwashukuru watanzania na wapishi wenzake kwa kumpigia kura nyingi na kuibuka mshindi katika kipengele cha mpishi bora mwanaume huku akisisitiza shauku juu ya elimu rasmi kwa kutumia lebo za reli kama vile #fanyaunachokipenda ("fanya unachopenda") na #chefmwabuki.
Chef Mwabuki ambaye kitaaluma ni askari wa wanayapori mwenye sifa zote aliwahi kuajiriwa na idara ya wanayamapori ambapo alifanya kazi kwa miaka kadhaa kwenye eneo la usimamizi wa wanyamapori,ambapo baadaye aliomba kuacha kazi hiyo kwa kuwa alisema yeye anapenda kupika zaidi na anaamini kwenye kufanya kitu anachokipenda.
Masama Blog inaungana na watanzania wote kumtakia kila la heri ana mafanikio zaidi Chef Mwabuki katika kuendeleza kazi zake za upishi pamoja na kuw ana huduma bora zinazoendelea kumletea wateja na kuwapa hamasa wengine wajue na kuona fursa zilizopo katika eneo la mapishi na huduma za chakula bora.