Mhandisi Makene Madoshi:Ni lazima tumuunge Mkono Rais Samia katika kutunza na kuhifadhi Mazingira

 

     Mhandis Dkt.Helladius Makene Madoshi

Mtaalamu mbobezi wa Masuala na tafiti na usimamizi wa Mazingira nchini Tanzania Dkt.Mhandisi Helladius Makene Madoshi amewataka watanzania kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha mazingira ya Nchi yetu kupitia maelekezo mbalimbali anayoyatoa yanaendelea kutunzwa na kuwa salama na oevu vikiwepo vyanzo vya maji  kwa ajili ya usatwi wa jamii na viumbe hai kwa ujumla.

Akizungumza jijini Mbeya wakati alipokuwa na semina ya uelimishaji jamii kuhusu umuhumu wa kulinda vyanzo vya maji na kupanda miti, katika mahojiano maalumu kuhusu nini kifanyike ili kuhakikisha mazingira ya kila siku ya watu na viumbe hai yanakuwa salama Dr.Madoshi amesema kwa sasa anafurahishwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kwenye maeneo mbalimbali zinakofanyka shughuli za kijamii zenye lengo la kuhifadhi mazingira tofauti na miaka ya nyuma ambapo eneo hilo halikuwa limetolewa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wake.

Aidha Mhandisi Madoshi amesema moja ya maeneo yanayotakiwa kuendelea kuwekewa kipaumbele na jamii ni pamoja na kuhakikisha utunzaji wa mazingira unakuwa jambo endelevu kwani ni moja ya kitu umuhimu kwa ajili ya Maisha ya kila siku ya viumbe hai.

Ikumbukwe Dkt. Heladius M. Makene ni mtaalamu wa mazingira na jamii nchini Tanzania, anayehusishwa na shughuli za usimamizi wa mazingira na maendeleo ya jamii katika sekta ya miundombinu na madini. Katika eneo la jamii na mazingira, Dkt.Madoshi amekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kampeni ya “Barabara na Mitaro siyo Jalala,” ambayo inalenga kuhamasisha wananchi kutunza miundombinu ya barabara kwa kuepuka kutupa taka ovyo.

Pia Dkt. Makene pia amehusika katika tafiti kuhusu athari za kijamii na kimazingira za sekta ya madini nchini Tanzania. Alishiriki katika utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Resources unaoitwa “Calling for Justice in the Goldfields of Tanzania,” ambapo alishirikiana na watafiti kutoka Clark University. Utafiti huo uliangazia changamoto zinazowakumba jamii zinazozunguka migodi ya dhahabu, hususan kuhusu haki za kijamii, mazingira, na ushiriki wa jamii katika maamuzi

Kwa ujumla, na hitimisho ni kwamba pamoja na kuwa mstari wa mbele katika masuala ya Mazingira bado Dkt. Heladius Makene anaendelea kuwa ni mmoja wa wataalamu wa mazingira nchini wenye uzoefu mpana katika masuala ya mazingira na maendeleo ya jamii, na mchango wake unaonekana katika jitihada za kuhakikisha maendeleo ya miundombinu na sekta ya madini yanazingatia ustawi wa jamii na uhifadhi wa mazingira.

Mwisho.

 


Previous Post Next Post

نموذج الاتصال