Ticker

10/recent/ticker-posts

SIMULIZI: Hakika Yalionikuta Maishani Ni Mengi - Sehemu ya Pili (02)


 Maafisa hao waliokuwa na nyuso zilizofadhaika walitabasamu walipoliona sanduku hilo likiwa salama na limefungwa kwa funguo kama lilivyokuwa lilipotoka benki.

Baada ya kulipakia kwenye gari walilokuja nalo walinipa mikono ya pongezi na shukurani.

“Tunakushukuru sana kwa ujasiri wako, umefanya kazi nzuri sana” Afisa mmoja akanimabia kwa furaha.

Polisi wanne waliofika hapo waliniuliza kulikoni. Nikawaeleza mkasa uliotokea. Baada ya kupata maelezo yangu walimtoa yule jambazi aliyekuwa amebanwa ndani ya lile gari nililolipindua. Alikuwa hoi. Damu ilikuwa inamtoka puani na mdomoni.

Hapo tukagawanyana kazi. Polisi wawili walisindikiza zile pesa kiwanda cha bia. Sisi wengine tulibaki pale pale tukiwasiliana na maafisa wetu.

Dakika chache tu baadaye polisi na makachero kutoka makao ya polisi walitinga katika eneo hilo.

Kila kachero na kila polisi aliyefika hapo alinipongeza kwa kazi nzuri, kuwaua majambazi wanne na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa za mishahara ya wafanyakazi wa kiwanda cha bia. Baadye ilibainika kuwa pesa hizo zilikuwa zaidi ya shilingi milioni mia tatu.

Majambazi niliowaua walipelekwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Muhimbili pamoja na yule polisi mwenzetu aliyeuawa. Jambazi aliyejeruhiwa baada ya kumpindua na gari naye alipelekwa kutibiwa katika hospitali hiyo hiyo akiwa chini ya ulinzi mkali.

SASA ENDELEA....

Siku ile ile niliitwa makao ya polisi. Niliambiwa kutokana na ujasiri niliouonesha wa kupambana na majambazi wanne na kuwaua na kuokoa pesa walizotaka kuzipora, nimehamishiwa katika idara ya upelelezi ya makosa ya jinai. Hivyo sitatumia tena sare za polisi bali nitakuwa nikivaa kiraia.

Mbali na kuhamishiwa katika idara nyingine ya kazi nilihamishiwa pia katika kituo kingine cha kazi. Kutoka kituo cha polisi Ilala nilipelekwa makao ya polisi.

Mabadiliko hayo yalinipa furaha na faraja na kwa upande wangu yalikuwa kama cheo kwani yalisogeza karibu na wakubwa.

Nikiwa katika idara hii ya upelelezi makao ya polisi ndipo jeuri yangu ilipoanza.

Pale nilikutana na makachero wenzangu vijana walionizidi kielimu. Tulikuwa tukivinjari katika mitaa ya jiji la Dar mchana kutwa.

Tulikuwa katika vikundi vikundi. Siku tunakuwa wawili, siku nyingine tunakuwa watatu. Kilichonifurahishani kuwa kila mmoja wetu alikuwa amekabidhiwa bastolayake kwa ajili ya kukabiliana na tukio lolote la kiusalama.

Nilipoanza kazi hii ya ukachero makao ya polisi nilibadilisha mavazi nikawa napendelea sana kuvaa koti. Watu wengi waliokuwa wananifahamu hawakujua ni kwanini nilikuwa sibandukani na koti. Wengi walidhani ni mbwembwe zangu. Lakini ukweli ni kuwa nilikuwa navaa koti ilikuficha bastola yangu na pia kupata urahisi wa kuitoa na kuitumia pale inapohitajika.

Nilipata rafiki kachero mwenzangu aliyeitwa Shaali Shazume. Alikuwa Mzanzibari aliyehamishiwa Dar kutoka Unguja.

Mimi na Shaali tulikuwa na tabia ya kutengeza kesi na kujipatia rushwa mara nyingi.

Lakini siku moja taarifa zetu zikatua kwenye mez ya mkuu wetu. Akatuita na kutuambia kuwa alikuwa amepata ushahidi juu ya tabia yetu ya kuwatengezea watu kesi na kula rushwa. Kutengeza kesi kulimaanisha kumbambikia mtu kesi.

Mimi na Shaali tulizikana tuhuma hizo na tukatolewa ushahidi ambao pia tuliukana kwa kudai kuwa ulikuwa ushahidi wa uongo.

Kukana kwetu kulitusaidia tusifukuzwe kazi lakini mimi na Shaali tukatenganishwa. Mimi nilihamishiwa mkoa wa Tanga na Shaali akapelekwa Tanga.

Sikuwahi kufika katika mkoa huo kabla ya hapo isipokuwa nilikuwa nikiusikia sifa zake. Na nilipoambiwa ninakwenda Tanga nilifurahi.

Nilifanya kazi Tanga kwa takribani mwaka mmoja. Nikagundua kuwa mkoa huo ulikuwa na watu wakarimu sana na pia ulikuwa na wasichana warembo sana.

Haukuwa mkoa wenye hekaheka kama ilivyo mikoa mengine ambapo polisin wanakuwa na mchakamchaka mchana wakati wote. Kusema kweli nilipokuwa Tanga nilitulia.

Kwenye kituo nilichokuwa nafanya kazi kulikuwa na sajenti mmoja ambaye alikuwa mtu wa nyumbani. Alisoma na kaka yangu Kagera.

Alikuwa ni sajenti Erick. Kachero huyo licha ya kunipenda alinichukulia kama mdogo wake. Mara nyingi alikuwa akinipa upendeleo wa kikazi. Siku za mapumziko nilikuwa namtembelea nyumbani kwake ambapo huzungumza na kukumbushana matukio ya kwetu Kagera.

Sikuwa nikijua kuwa nilikuwa namtengeza Shaali mwingine badala ya yule niliyekuwa naye Dar kwani baada ya miezi michache tu yalitufika makubwa.

Kuna siku nilikuwa kwenye mizunguko yangu ya kikazi. Sajenti Erick akanipigia simu. Nilishituka nilipoonanamba yake kwa sababu hakuwa na kawaida ya kunipigia simu.

“Shikamoo afande” nilimuamkia ,mara tu nilipopokea simu yake.

“Marahaba Martin. Uko wapi muda huu?” akaniuliza kwenye simu. Martin ndio jina langu. Jina langu kamili ni Martin Philip Lazaro.

“Niko eneo la stendi ya mabasi” nikamjibu.

“Kuna nini huko?”

“Naangaza kwenye mabasi yanayotoka Mombasa. Naweza kushika mirungi”

“Sasa umefanikiwa?”

“Hakuna kitu, nataka kurudi kituoni”

“Hebu njoo hapa hoteli ya Mtendele”

Mtendele ni hoteli moja maarufu iliyoko eneo la Chuda.

“Wewe uko hapo?”

Sikutaka kumuuliza kuna nini. Nilikodi bodaboda ikanipeleka Mtendele. Nilipoingia nilimkuta Erick akinywa bia.

Kiumri alikuwa amenizidi kwa miaka isiyopungua minane.

“Kaa hapo” akaniambia akinionesha kiti kilichokuwa kwenye meza aliyoketi.

“Najua huna pesa, nataka nikupe kazi lakini uwe ngangari” akaniambia mara tu nilipoketi kwenye kiti hicho

“Sawa”

“Nimepata taarifa moja, kuna mama mmoja na binti yake wana duka la vitu vya dhahabu na mapambo ya wanawake pale barabara ya nane kwa barabara ya jamaa”

“Ana nini huyo mama?” nikamuuliza.

“Nataka twende tukapekue nyumbani kwake, nimesikia anajishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya. Lile duka ni danganya toto tu”

“Sawa. Twende tukafanye hiyo kazi”

“Ngoja nimalize bia yangu twende”

“Si itabidi twende kituoni tukaandike hati ya upekuzi”

“Hapana, twende hivi hivi tu. Si kila kitu kinahitaji hati ya upekuzi. Kwanza watu wenyewe ni wanawake, hawajui sheria yoyote”

“Sawa”

Erick akamaliza bia yake na kuinuka.

Itaendelea Kesho usikose kuitembelea Blog Hii.

Post a Comment

0 Comments