Ticker

10/recent/ticker-posts

TARURA Yaendelea Kufungua Barabara za Ruangwa na Mkoa wa Lindi.Soma hapa

Lindi

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Lindi imekamilisha ujenzi wa daraja la Mbwemkuru lenye urefu wa mita 75 na kufungua barabara ya Ruangwa-Nangurugai- Kiangara-Mirui-Mbwemkuru yenye jumla ya Km 65.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Ruangwa, Mhandisi Mashaka Narubi ameeleza kuwa kukamilika kwa daraja hilo imekua ni fursa kwa wananchi kusafiri kwa urahisi kutoka Ruangwa kwenda Liwale.

"Daraja hili ni muhimu kwa wananchi wa wilaya zote mbili katika kusafiri na kusafirisha bidhaa na mazao, tumejenga daraja na kufungua barabara na sasa magari yanapita hapa kwenda Liwale ", amesema mhandisi Narubi.

Naye. Bi Sharifa Majaliwa mkazi wa Kijiji cha Nangurugai amesema kuwa kabla ya kujengwa Daraja hilo ilikuwa vigumu kwao kufanya shughuli za kilimo ng'ambo ya pili ya mto lakini kwa sasa wanavuka na kufanya kazi zao kwa urahisi.

"Kutoka hapa Nangurugai kwenda Mirui ilikua ni vigumu, mto una mamba na tulikua tukivuka kwa kutumia njia hatarishi lakini sasa tunashukuru Serikali kwa kukamilisha daraja hili, amesema Bi Sharifa.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mirui, Bw. Chande Ally amesema kuwa mwanzoni Kijiji hicho kilikuwa hakifikiki kwani mtu alikuwa hawezi kutoka Mirui kwenda Ruangwa kwa urahisi.

"Kijiji chetu kilikua Kisiwani, ufunguzi wa barabara hii na kukamilika kwa daraja la Mbwemkuru limefunguwa fursa kubwa za kiuchumi na kijamii", amesema Bw. Chande.

Naye kwa Upande wa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)  Mhandisi Victor Seff aamesema barabara za Mkoa wa Lindi zikiwepo Mikoa mbalimbali ni mwendelezo wa kazi za Wakala katika kusimamia Matengenezo ya Barabara Mbalimbali zikiwepo ahadi za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Utekelezaji wa ilano ya Chama Cha Mapinduzi na kazi inaendelea kufungua barabara katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwezesha wanachi kufika kusikofikika.

Post a Comment

0 Comments