Ticker

10/recent/ticker-posts

Hawa Hapa Ndio Watanzania Wenye Followers Wengi Huko Twitter

 

Millard Ayo (2.4M Followers)
Ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa Clouds Media, pia ndiye mmiliki wa Ayo tv

Mohammed Dewji (1.9M Followers)
Tajiri namba moja Tanzania ambaye ni mfanyabiashara na muwekezaji wa Simba Sport Club mwenye hisa 49% lakini kila siku analalamika timu inampa hasara (Sasa kina Sawadogo watampaje faida? 😂)

Masoud Kipanya (1.9M Followers)
Mtangazaji wa Clouds Media na mchoraji katuni ngumu kutafsirika hasa kwa wenye ubongo wa mende kama wangu

Jakaya Kikwete (1.7M followers)
Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Zitto Kabwe (1.6M followers)
Mwanasiasa na Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo

Samia Suluhu Hassan (1.4M followers)
Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Diamond Platinumz (1.3M followers)
Mwanamuziki, Mfanyabiashara na mmiliki wa Wasafi Media

Maulid Kitenge (1.3M followers)
Mtangazaji wa Wasafi Media na mmiliki wa Kitenge TV

Idris Sultan (1.3M followers)
Mshindi wa BBA (Big Brother Africa) mwaka 2014 ambaye pia ni mchekeshaji na muigizaji wa filamu bongo na nje ya nchi

Kigogo, Makamba & Maria Sarungi (1.2M followers)

Wengine ni Fatma Karume, Dk Hamis Kigagwala, Jokate Mwegelo, Masanja Mkandamizaji, Madenge, Roma Mkatoliki na wengineo

Post a Comment

0 Comments