Ticker

10/recent/ticker-posts

Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo Kuliteka Jiji la Mbeya, Atanguruma Kuanzia Saa Saba Mchana leo

Katibu Mkuu wa Chama Chama Mapinduzi Ndugu Daniel Godfrey Chongolo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara wa chama cha mapinduzi (CCM) utakaofanyika jijini Mbeya leo 15/07/2023  kuanzia saa saba kamili Mchana katika uwanja wa Rwandanzovywe uliopo Ilomba jijini humo...Mkutano huo pia utarushwa Mubashara(LIVE) na vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuanzia saa 7 mchana.

Hii ni moja ya mikutano ya hadhara ambayo amekuwa akiifanya Ndugu Chongolo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kukagua na kukiimarisha chama cha mapinduzi kuazia ngazi ya Shina na tayari mikutano kama hii imeshafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam,Tanga,Iringa,Kilimanjaro,Manyara,Dodoma na kwingineko ambapo Moja ya jukumu kubwa analofanya Chongolo ni kuwasisitiza na kutoa maelekezo kwa watendaji wa serikali ya kusikiliza na kuzitatua kero za waananchi kwa wakati kama iliyoainishwa katika ilani ya CCM.

Post a Comment

0 Comments