Ticker

10/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS: BERNARD MEMBE AFARIKI DUNIA,RAIS SAMIA ATUMA RAMBIMRAMBI

 

Mwanadiplomasia na Mwanasiasa mkongwe aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Marehemu Bernard Membe amefariki asubuhi leo jijini Dar es Salaam katika hospitali ya Kairuki alikofikishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma ujumbe wa rambi rambi kwa familia na taifa kwa ujumla  kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benard  Camilius Membe, aliyefariki dunia asubuhi leo Ijumaa wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Kairuki, Jijini Dar-es-salaam.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter, rais Samia amemtaja Membe kuwa mtumishi wa umma aliyefanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu kama mwanadiplomasia, mbunge na waziri aliyeitumikia nchi yake kitaaluma.

Benard Membe alikuwa waziri wa mambo ya nje ya Tanzania kati ya mwaka 2007 na 2015, wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

Umaarufu wa Benard Membe kisiasa ulianza mwaka 2000 alipochaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la  Mtama mkoani Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM. Alishinda kiti hicho tena mwaka 2005 na 2010.

Benard Membe, ambaye alisomea Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa katika chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani na pia alikuwa mtaalam wa maswala  mbalimbali katika ofisi ya Rais kabla ya kuwa mbunge.

Alihudumu katika nafasi mbali mbali nchini Tanzania ikwemo naibu waziri wa nishati na madini lakini alifutiwa uanachama wa CCM mwaka 2020, kwa madai ya kinidhamu na kuvunja kanuni na katiba ya chama lakini baadaye alisamehewa na kurudishiwa uanachama wake wa CCM chini ya Mweneyekiti wake wa sasa Rais Samia Suluhu Hasssan na uongozi wa sasa wa chama hicho
Taarifa za kinachoendelea tutaendelea kukuletea kupitia blog yetu hii..

PUMZIKA KWA AMANI MWANADIPLOMASIA BERNAD CAMILIUS MEMBE

Post a Comment

0 Comments