Ticker

10/recent/ticker-posts

WAZIRI ANGELLAH KAIRUKI:RAIS SAMIA AMETOA KIBALI CHA KUAJIRI WATUMISHI 21,200 AFYA NA ELIMU,ONA NAFASI ZOTE HAPA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki akizungu

Na.  Angela Msimbbira OR-TAMISEMI 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ametangaza nafasi  za ajira 21,200  kwa kada ya Walimu na Afya.

Akitoa taarifa  kwa vyombo vya habari Aprili 12, 2023 Jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki  amesema idadi ya watakaoajiriwa katika kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika  shule za msingi na Sekondari na kada ya afya 8,070 watakaofanya kazi katika Hospitali za Wilaya, Vituo vya afya na Zahanati

Waziri Kairuki amesema  mchakato wa kuajiri  watumishi hao umeanza   Aprili 12 ,2023 hadi  Aprili 25, 2023 ambapo waombaji wa nafasi za ajira katika hkada ya ualimu na afya  wanatakiwa  kuwa wamehitimu  kwenye vyuo  vya elimu ya juu na kati kwenye fani ya ualimu na afya vinavyotambuliwa na Serikali.

Ameendelea kufafanua kuwa nafasi zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate),  stashahada (Diploma) na shahada (Degree) ambapo sifa za kitaaluma zimeanishwa kwa waombaji wa kada za ualimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na fani mbalimbali za kada ya afya kama zilivyoainishwa katika tangazo la ajira  na katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI 

Amesema waombaji  wa kada ya ualimu wawe wamehitimu kuanzia mwaka 2015 hadi 2022 na kwa kada ya afya wasizidi umri wa miaka 45, hivyo amewataka waombaji hao kuanza kutuma  maombi  yao kuanzia leo  tarehe 12 Aprili, 2023 hadi   25 Aprili, 2023 saa 5:59 usiku.

Waziri Kairuki amewataka waombaji waliowahi kutuma maombi ya ajira kupitia mfumo wa maombi ya ajira  kuhuisha taarifa zao  kwenye  mfumo wa ajira kupitia kiunganishi ajira.tamisemi.go.tz kwa kutumia namba ya mtihani wa kidato cha nne na nywila au kuomba upya .

Amewataka waombaji wa ajira hizo kuwa tayari kufanyakazi kwenye Halmashauri na vituo watakavyopangiwa, kufanyakazi na mashirika au taasisi zilizoingia ubia na Serikali na baada ya kupangiwa kituo cha kazi hakutakuwa na nafasi ya kubadilishiwa kituo cha kazi 

Aidha ametoa rai kwa waombaji wa ajira hizo kupeuka matapeli watakaowapigia simu na kuwataka kutoa fedha kwa ajili ya kupata ajira kwa kuwa ajira hizo ni bure, vigezo na masharti vitatumika katika kuwaajiri watumishi hao

“Natoa rai kwa waombaji, mtu asije akapigiwa simu kuombwa fedha kwa ajili ya kupata ajira hizo, msiingie katika huo mtego kwa kuwa ikibainika  hilo limejitikeza  toeni taarifa kwa Mamlaka ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya matapeli” amesisitiza Waziri Kairuki.


BONYEZA HAPA KUONA NAFASI MPYA ZA KAZI  ZAIDI 21,000 ZA UALIMU NA AFYA ZILIZOTANGAZWA 2023

Post a Comment

0 Comments