Ticker

10/recent/ticker-posts

RC MAKALA NA DC MPOGOLO WAZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MITI ZAIDI YA MILIONI MOJA WILAYANI ILALA DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makala pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam Mhe.Edward Mpogolo (Picha mbalimbali zikiwaonyesha walipozindua kampeni kabambe ya upandaji miti wilayani Ilala) ambapo Mhe.Edward Mpogolo amesema amezindua kampeni Rasmi ya upandaji miti wilayani ilala jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kupanda miti Milioni moja na Laki tano.


na waandishi wa wa habari wa kituo cha ITV/Radio one jijini humo jana katika mahojiano maalumu Mheshimiwa Mpogolo amesema kupanda miti ni zoezi endelevu na lengo ni kufikia upandaji wa miti mipya isiyopungua milioni moja na nusu na kama inavyofahamika miti ni vyanzo vya mazingira nadhifu,hali ya hewa,matunda,vyanzo vya maji nk.

hatua nyingine ya kuonyesha kuwa zoezi hilo ni endelevu DC Mpogolo amesema pia ameanzisha shindano la kupanda miti kwa shule zote za wilaya ya ilala ambapo pia shule itakayofanya vizuri kwa kupanda miti mingi na kuituza watatunukiwa zawadi maalum kwa kutambua mchango wao katika kutunza mazingira huku akiwasisitiza waandishi hao (Maulid Kambaya) na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari  wawe mabalozi wema wa kusaidia kuelimisha jamii juu ya umuhimu kampeni hiyo yenye manufaa kwa wilaya ya ilala na taifa kwa ujumla kwani uwepo wao katika vyombo vya habari una mchango mkubwa wa kusaidia kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu kampebni hii.


Aidha Mhe.Mpogolo amewasisitiza wananchi wa wilaya ya Ialala na Dar es Salaam kwa ujumla kujitahidi kwa kuhakikisha kila mtu anakuwa balozi wa mazingira kwa kuopanda miti katika maeneo yake kwani kufabya hivyo ni kuendeleza uhai wa mazingira safi na rafiki kwa wilaya ya Ilaala na Jiji la Dar es Salaam kwa Ujumla.

Post a Comment

0 Comments