Ticker

10/recent/ticker-posts

MSIKIE MHE.ROSEMARY SENYAMULE BAADA YA MHE.RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUCHAGULIWA KUWA MWNYEKITI WA CCM TAIFA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary S. Senyamule amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa Kuchaguliwa na Mkutano Mkuu CCM Taifa kuwa mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka mitano 2022-2027 na kusema amefurahishwa sana na kuupongeza uamuzi wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 10 wa CCM Taifa kwa kumchagua kwa kura za kishindo.Katika Mazungumzo yake na wana habari leo Mkuu wa Mkoa huyo Mhe.Rosemary Senyamule amesema.....

''.....Kwa  kweli Nampongeza sana Mhe.Rais wetu kwa ushidi huu..na niseme wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa wamenifurahisha sana kwani wamefanya maamuzi sahihi,wakati sahihi na kwa watu sahihi ambapo  kwa kumchagua kwa kishindo Rais Samia, Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa,Ndg.Abdulrahman Omar Kianana kuwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara na Ndugu. Hussein Ali Mwinyi kuwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Visiwani,na sisi kama wateule wake na wasidizi wake tunaahidi kuendelea kuchapa kazi bila kulala kuhakikisha dhamira ya Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Rais Samia kwa wananchi wa dodoma na watanzania inafikiwa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM pia.....''


Post a Comment

0 Comments