Ticker

10/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU DANIEL CHONGOLO AFUNGUKA KUHUSU MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA 2022

Kwanza kabisa kama mjuavyo wapenzi wasomaji wetu tarehe 7- 8/12/2022 ni siku za mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe wa mkutano mkuu huo wanaotarajiwa kuwa zaidi ya 1900 watafanya uchaguzi wa Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Hicho.

Viongozi Mbalimbali wakiwepo wabunge,Makada wa chama hiki kikongwe wameonekana kuwakaribisha wajumbe hao wa mkutano mkuu wa 10 wa Taifa utakaoongozwa na mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Aidha akizungumzia maandalizi ya Mkutano mkuu huo wenye hamasa na mvuto mkubwa ikiwa ni mkutano mkuu wa kwanza kwa mwaka 2022 baada ya chaguzi za ngazi mbalimbali za ndani za chama hicho  Katibu Mkuu wa CCM Mhe.Daniel Chongolo amesema Kila kitu kinaenda vizuri na hatua nyingi muhikmu za maandalizi zimekamilika..

''..Mkutano wetu Mkuu wa 10 utakaoongozwa na Mwenyekiti wetu Ndugu Samia Suluhu Hassan unatarajiwa kupokea wajumbe toka mikoa yote kama ilivyo kawaida na kama ilivyo desturi ya chama chetu tutahakikisha tunakamislisha mambo yote kwa wakati kwani hadi sasa maandalizi yanakwenda vizuri na Mimi binafsi nawakaribisha sana Wajumbe wote na wageni Mbalimbali katika mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Mapinduzi utakaofanyka katika ukumbi wetu wa kituo cha Mikutano cha  Jakaya Kikwete Convention Center (JKCC)  Jijini Dodoma unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 na 8 Disemba..'' Alimalizia Chongolo.

Post a Comment

0 Comments