Ticker

10/recent/ticker-posts

TUSICHANGANYE MADESA


Picha Hii ilitumika kwa mara ya kwanza April 17,2015  na mtandao wa New times.Picha hii imetumika sana katika kipindi cha vurugu zilizokuwa zikifanyika Afrika kusini mwanzoni mwa Septemba mwaka huu ikilinganishwa na matukio hasa ya vurugu.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
KUTOKUJUA sheria sio kinga ya kuvunja sheria, hivyo basi tusichanganye madesa wakati wa matukio mbalimbali yanapotokea duniani kote.

Katika Vurugu za Afrika Kusini zilizoanza mwanzoni mwa septemba, 2019 msanii na mzazi mweza wa msaani wa Bongo freva Nasib Abdul maarufu kama Diamond, Zarina Hassani kwenye akaunti yake ya Instragram aliweka picha iliyounganishwa na kuhusisha picha hiyo na vurugu zilizotokea mwanzoni mwa Septemba mwaka huu nchini Afrika Kusini

Hat hivyo picha hiyo  kwa mara ya kwanza ilipostiwa 17Aprili 2015 saa 12:26 ikiwa na kichwa cha habari  cha Why are South Africans attacking fellow Africans? ambapo picha iliyowekwa ni kipindi cha mwaka 2015 na watu kuchukua kuitumia kwa vurugu za 2019.

Baada ya hapo picha hiyohiyo ililudiwa kupostiwa na mtandao wa 
nehandaradio.com Novemba 2,2017 mwandishi wa aliandika makala kuelezea matatizo ya mapigano ya Afrika kusini.

Hata hivyo habari za uongo zimekuwa kikitamaraki katika mitandao ya kijamii bila kujua chanzo cha picha pamoja na video ambazo hazihusiani na matukio na kuhusisha ma tukio linalokuwa linaendelea kwa kuchochea hisia za hasira za watu kufanya vitendo ambavyo hawakuvitegemea kutokana na picha tuu ambazo haziendani na mazingira husika.

Hata hivyo picha hiyo imeweza kutumika na mitandao mbalimbali kama The new times ilitumika 2015, Zambianobserver.com walitumia Machi, 29,2018, Afrigue.le360.ma walitumia picha hiyohiyo Oktoba 27,2019 wakihusisha picha hiyo na vurugu zilizokuwa zikiendelea Afrika Kusini mwanzoni mwa Septemba Mwaka huu.

Basi sasa kama mtu akiwa anatuma picha kwenye mitandao ya kijamii awe na uhakika na picha anayotuma ili kuondokana na kupunguza kabisa habari za uzushi(Fake News).


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2VJoMqs
via

Post a Comment

0 Comments