Ticker

10/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHE. CONSTANTINE KANYASU AONYA WAHARIBIFU WA MISITU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akinyosha mikono kuwasalimia Wachimbaji wadogo wa madini kabala ya kuanza kuzungumza na Wachimbaji hao kwenye mkutano mkoani Geita uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali. 
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanlaus Nyongo akizungumza na Wachimbaji wadogo wa madini kwenye mkutano uliofanyika mkoani Geita uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali. 
Baadhi ya Wachimbaji Wadogo wa madini wakiwa kwenye mkutano uliofanyika mkoani Geita uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanlaus Nyongo wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wachimbaji Wadogo wa madini wa wilaya Mbogo mara baada ya Naibu Waziri Madini, Mhe.Nyongo kufunga mkutano huo uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha ,mali 
Mkurugenzi Mwezeshaji wa kutoka MKURABITA,, Dkt. Anastazia Haule akizungumza na Sachimbaji Wadogo wa Madini kabla Naibu Waziri Madini, Mhe.Nyongo kufunga mkutano huo uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha ,mali 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhe. Leonard Bugomola akizungumza na Wachimbaji Wadogo wa madiini kuhusu umuhimu wa kujiunga katika vikumdi ili waweze kukopesheka. ( Picha zote na Wizara ya Maliasili na Utalii)

…………………….. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema Tanzania kwa mwaka mmoja inateketeza takribani hekta 400,000 za misitu ambapo endapo hali hii itaachwa hivyo Misitu iliyopo nchini itaisha baada ya miaka 12 

Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amesema Wizara yake itaendelea kulinda misitu hiyo kwa nguvu zake zote ili kuweza kuinusuru. 

Hayo ameyasema mkoani Geita wakati alipokuwa akizungumza na Wachimbaji Wadogo wa madini kwenye mkutano uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali. 

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe.Kanyasu amesema shughuli za uchimbaji madini zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa katika uteketezaji wa misitu hiyo. 

Amesema Wachimbaji walio wengi wamekuwa ni watu wa kuhama hama na kila mahali wanapohisi kuna madini wamekuwa wakifyeka misitu bila kujali athari zake.. 

Ameongeza kuwa kwa vile Wachimbaji hao wamekuwa wakifyeka misitu hiyo katika maeneo makubwa hata baada ya kumaliza uchimbaji huo hushindwa kupanda miti mingine. Amewaeleza kuwa madhara yake ni makubwa na kama hali hiyo itaendelea kwa vile mara baada ya misitu hiyo kuisha mvua hazitaweza kunyesha na hali ya maisha itakuwa ngumu sana. 

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka Wananchi wanaokata miti iwe yao walioyaipanda uwe mwembe au mti wa aina yeyote wafuate taratibu za kupata kibali kwa Maafisa misitu au wenyeviti wa maeneo husika. Amesema kwa wale wanaokata miti hiyo bila kupata kibali kwa mamlaka husika, Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria. 

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Mhe. Stanlaus Nyongo amewataka Wachimbaji hao kufuata sheria pale wanapohisi uwepo wa madini katika maeneo ya Hifadhi .Amewataka watoe taarifa kwa Wamiliki wa Hifadhi kwa ajili ya kupata idhini badala ya kuanza kuvamiwa maeneo hayo kwa kuanza kufyeka misitu. 

Naye, Hamisi Abdala aliyejitambulisha kama Mchimbaji mdogo amesema atakuwa Balozi kwa Wenzake kwa kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kulinda misitu.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2jJDCyT
via

Post a Comment

0 Comments