Ticker

10/recent/ticker-posts

TANZANIA NA KENYA WAANZA KUJADILI KUONDOA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA MIPAKANI

Na Ahmed Mahmoud Longido

Mawaziri wa Kenya na Tanzania wamekutana kutatua changamoto za mipakani Kati ya nchi hizo mbili ili kuongeza ufanisi na kuondoa changamoto Kwa Wafanyabiashara wa pande hizo mbili.

Mawaziri wa Biashara kutoka nchi za Kenya na Tanzania wamekutana kujadili na kutatua changamoto za kibiashara katika mipaka ya nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuskiliza kero za wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi ili kuondokana na usumbufu wanaoupata wafanyabiashara.

Wafanyabiashara hao wameeleza changamoto ya mizigo yao kukaa muda mrefu mipakani humo pamoja na changamoto ya hati za muda za kusafiria madereva kutolewa kwa muda mfupi hivyo kuathiri biashara hivyo wameomba hati hizo zitolewe kwa muda wa mwaka mmoja na si kwa safari moja pekee 

Waziri wa biashara nchini Kenya Chris Kibito amesema kuwa asilimia 45% ya biashara ya afrika mashariki inafanyika kati ya Tanzania na Kenya hivyo ni vyema kuimarisha mahusiano ya kibiashara ili nchi zote mbili ziweze kunufaika pia ameahidi kushughulikia kwa karibu changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara mipakani humo 

Amesema kuwa mbali na biashara kuchelewa mipakani kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo suala zima la upimaji wa viwango vya bidhaa zinazovuka watajitahidi kuhakikisha masuala yote yanatatuliwa ndani ya miezi mitatu.

Amesema malengo ya biashara ni kukuza uchumi Kwa upande mmoja na hivyo kama suala hilo halikuchukuliwa Kwa kuliangalia Kwa ndani kuondoa changamoto basi hatutapiga hatua kiuchumi.

Waziri wa biashara na viwanda nchini Tanzania JOSEPH KAKUNDA amesema kuwa changamoto zilizofikishwa na wafanya biashara hao wanazifanyia kazi kwa kushrikiana na maslahi mapana ya nchi zote hivyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuwa na uvumilivu wakati wakisubiri majibu ya changamoto hizo.

Amesema kuwa hakuna nchi hata moja ambayo inataka kuona changamoto za kibiashara kwenye mipaka hivyo ndio maana wamekutana kujadili na kuona namna nzuri ya kuondoa changamoto za kibiashara mipakani mwa nchi hizo

Mawaziri kutoka nchi za Kenya na Tanzania wameweka saini ya makubaliano ya kukutana mara mbili kwa mwaka ili kutatua changamoto za kibiashara na kuimarisha mahusiano.



from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2XNMF00
via

Post a Comment

0 Comments