Ticker

10/recent/ticker-posts

Mimi Sijawahi kuwa na ‘kibenteni’ zaidi ya Bond - Wastara

Msanii wa Filamu nchini, Wastara Juma amesema kuwa watu wasikariri kuwa yeye ni mtu kuwa katika mahusiano vibenteni zaidi ya aliyekuwa mpenzi wake Bond Bin Sinan. 

Wastara amesema kuwa yeye anapenda mtu amzidi mwaka mmoja ikiwa miaka miwili iwe kwa bahati mbaya. 

"Sijawahi kuwa na Kibenteni zaidi ya Bond Bin Sinan na yeye pia amenizidi mimi miaka miwili amezaliwa 81 mimi nimezaliwa 83 kwahiyo naweza sema muonekano wangu wa mwili unaniponza lakini sinaga mahusiano ya namna hii," Wastara ameiambia EATV. 

"Mimi napenda mtu anizidi na nikimzidi uwe mwaka mmoja miaka miwili tena kwa bahati mbaya yaani imetokea tokea tu tumekutana kwenye mahusiano kama ilivyokuwa kwa Sajuki hayakuwa rasmi lakini yalikuja kutengeneza mpaka ndoa."