Ticker

10/recent/ticker-posts

CCM Hatari kila Kona..Soma hii Taarifa Mpya Toka kwa Mbunge wa Dodoma(CCM)Mhe.Anthony Mavunde..

Image may contain: 1 person
TULIAHIDI NA SASA TUNATIMIZA

Kesho saa 3 asubuhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni Rasmi katika Hafla fupi ya uzinduzi wa Mpango wa Ugawaji wa Ipad 5000,laptops na projectors kwa Shule 10 zilizopo ndani ya Jimbo la Dodoma Mjini.

Ipad "vishkwambi" hizo ambazo zitakuwa zinahifadhiwa mashuleni,zitawekwa vitabu vya kusomea ambavyo vinaenda sambamba na mtaala wa elimu ya msingi na hivyo kumrahisishia mwanafunzi namna bora ya kujisomea vitu vingi kwa wakati mmoja.

Ninaamini kupitia mpango huu wa matumizi ya kiteknolojia ya kisasa itasaidia kuwafanya wanafunzi wengi zaidi kushiriki katika kujisomea na hivyo kusaidia kuongeza maarifa zaidi miongoni mwa wanafunzi.

Anthony Peter Mavunde
Mbunge Jimbo la Dodoma Mjini

Mtumishi wa watu "De populo servorum"