Ticker

10/recent/ticker-posts

Mwanamuziki JUX Akana Kuachana na Vanessa Mdee..Afunguka Haya

Muimbaji wa muziki wa R&B, Jux amefunguka kwa kusema kuwa bado yupo kwenye mahusiano ya mapenzi na Vanessa Mdee.
Jux and Vanessa Mdee

Wawili hao wameacha tabia ya kushare picha zao katika mitandao ya kijamii na kuibua tetesi kuwa huwenda wameachana.

Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Alhamisi hii, Jux ameizima tetesi hiyo kwa kusema bado yupo kwenye mahusiano na muimbaji huyo wa kike wa wimbo Niroge.

“Tumefika kipindi ambacho tuyaweka mahusiano yetu privacy na mziki wetu uendele,” alisema Jux “Bado mimi na Vanessa Mdee ni wapenzi,”

Pia Jux amewataka mashabiki wa muziki wake kusupport wimbo yake mpya ‘Wivu’ ambao ameuachia hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments