Ticker

10/recent/ticker-posts

Picha: TRA Wanaipiga Mnada Range Rover Evoque ya Wema Sepetu


Unaikumbuka ile Range Rover Evoque 504 ambayo Wema Sepetu alijizawadia kwenye birthday yake mwaka jana?

Well, inaweza kuwa yako iwapo unaweza kuwa na takriban shilingi milioni 200 za kumwaga sababu TRA wanaipiga mnada!

Picha hapo juu Range Rover Evoque ya Wema Sepetu ikiwa kwenye yard za TRA ikipigwa mnada

TRA wanaishikilia gari hiyo kwasababu iliingizwa nchini bila kulipiwa kodi na kwakuwa ushuru wake ni takriban nusu ya gharama yake, Wema ameshindwa kuikomboa.

Kuna tetesi ziliwahi kuandikwa kuwa gari hilo hata hivyo alipewa kama zawadi na pedeshee wa Kongo anayedaiwa pia kuwahi kuwa na uhusiano na Jacqueline Wolper.