Ticker

10/recent/ticker-posts

MUONE HUYU SHAROBARO AKIWA ANAKULA RAHA NA HAUSIGELI LIVE

Issa Mnally na Richard Bukos
KIJANA mmoja mtanashati, aliyefahamika kwa jina la Faraja Adam mkazi wa Makongo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alinusurika kipigo kutoka kwa wakazi wa Mabibo Jeshini baada ya kukutwa sebuleni kwa mpangaji wa nyumba moja aliyefahamika kwa jina la Rhobi Chacha.
Majirani wa mpangaji huyo waliliambia gazeti hili kwamba walimuona kijana huyo akiambaaambaaa na ukuta wa nyumba hiyo kisha kuingia ndani kwa kunyata, kitu kilichowapa shaka na kuamua kumpigia simu jirani yao kumweleza juu ya ujio wa kijana huyo.
Majibu waliyopewa na mpangaji huyo yaliwafanya majirani hao kujikusanya, wakiwemo walinzi wa kimasai wanaolinda maeneo hayo na alipofika Rhobi, ndipo walipoingia ndani na kupigwa na butwaa kumkuta ‘sharo’ huyo akiwa amejilaza kwenye kochi sebuleni, akiwa ameshikilia rimoti akiibonyezabonyeza kama yupo nyumbani kwao.
Alipoulizwa kilichompeleka hapo, alikosa cha kujibu, akionekana kuchanganyikiwa. Baada ya kutishiwa kipigo cha kumwitia mwizi kwa kuingia kwa watu bila wenyewe kuwepo, aliomba aachwe kwa maelezo kuwa alimfuata dada wa kazi wa nyumba hiyo.
“Jamani mimi nina ndugu zangu wakubwa sana serikalini, naomba msinifanye chochote kile, nimekuja kwa Jesca (house girl) kwani ni dadangu kabisa,” alijitetea kijana huyo.
Jesca baada ya kuulizwa uhusiano wake na kijana huyo alikosa cha kusema, lakini simu yake ya mkononi ilipopekuliwa, ilikutwa ikiwa na meseji alizokuwa akitumiana na kijana huyo, zilizoashiria mapenzi.
Baadaye wawili hao walidhibitiwa na kupelekwa kituo cha Polisi cha Urafiki ambako mzazi wa Faraja alipoitwa, alitaka mwanaye huyo alazwe rumande ili iwe fundisho kwake aachane na tabia hiyo.
Naye Rhobi, aliliambia gazeti hili kuwa tabia ya msichana wake huyo wa kazi imebadilika katika siku za hivi karibuni na kwamba mara kadhaa, amekuwa akikuta kitanda chake kikiwa kimevurugika tofauti na alivyokiacha

Post a Comment

0 Comments