TAYARI
imebainika kwamba, baadhi ya viongozi walioonesha nia ya kugombea urais
mwaka huu wameanza kupigiwa debe na wake zao ndani ya mitandao ya
kijamii ili waume hao watakapoibuka na ushindi wapate nafasi ya ‘u–First
Lady’, Risasi Jumamosi linakupa zaidi!Taarifa zilizotua juu ya dawati
la gazeti hili juzi zilisema kuwa, vita ni nzito kwani baadhi ya wake wa
wagombea nao wapo ndani ya mkakati wa kukusanya watu wa kuwaunga mkono
waume zao katika kinyang’anyiro hicho kitakachochukua nafasi Oktoba,
mwaka huu.
Wakati
vita hiyo ikiwa imepamba moto, mnajimu maarufu nchini, Maalim Hassan
Hussein naye ameibuka kwenye Risasi Jumamosi na kuanika utabiri mzito
juu ya wasifu wa mtu atakayeshinda urais huo.
HALI ILIVYO SASA
Habari
zinadai kuwa, baadhi ya wake wa viongozi hao nao wamekuwa wakipita
chini kwa chini kukusanya na kuweka sawa makundi ya kisiasa tayari kwa
kampeni za kuwaingiza ikulu waume zao.
ISHU NI KUMRITHI MAMA SALAMA KIKWETE
“Kila
mke wa mgombea anafanya kampeni za chini kwa chini. Unajua wenyewe kila
mmoja anafahamu kwamba ‘mzee’ akiingia ikulu yeye atakuwa First Lady
kumrithi wa sasa (mama Salma Kikwete), ndiyo maana siku hizi karibu wake
wa wagombea wote wana safari za mikoani kupanga timu ushindi,” kilisema
chanzo kimoja.
Mke wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.
FARAJA KOTA YUKO WAZI ZAIDI
Miss
Tanzania 2004, Faraja Kota ambaye ni mke wa Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu aliyetangaza nia, amekuwa akitupia maneno yenye
kumpigia kampeni mumewe huyo kwenye Instagram na mitandao mingine ya
kijamii.
KWENDA NAYE KANISANI
Desemba
mwaka jana, Faraja aliongozana na mumewe huyo ambaye pia ni Mbunge wa
Singida Kaskazini kwenda kwenye Kanisa la FPCT, Ilongelo na baadaye
kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, Singida ambako mumewe alitangaza
rasmi nia yake ya kugombea urais.
MAMA PINDA
Tunu
Pinda ni mke wa Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda. Yeye aliwahi
kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema alishtushwa kusikia
habari kwamba, mumewe ametangaza nia ya kugombea urais 2015.
Alisema
alipomuuliza mumewe alimwambia hajaita vyombo vya habari kusema hivyo
lakini muda ukifika atafanya hivyo. Mama Tunu akasema na yeye
anakubaliana na maneno ya mumewe kwamba muda ukifika atangaze kugombea
urais.“Kwa hiyo kama alivyosema na iwe hivyo kama Bwana Mungu aishivyo,
nasema amina. Kwa sababu muda bado haujafika, utakapofika tutajua,”
alisema mama Pinda.
YA MTABIRI SASA
Kuhusu
utabiri wa Maalim Hassan, amesema mwaka huu, Tanzania itampata rais wa
aina yake kuliko miaka yote iliyopita tangu uhuru (Desemba
9,1961).Akizungumza na gazeti hili Jumatano iliyopita, ofisini kwake,
Magomeni, Dar, Maalim Hassan alisema kuwa, rais atakayepatikana mwaka
huu atakuwa mtu aliyechanganya dini.
Alisema mtu huyo, kama baba yake atakuwa Muislam basi mama atakuwa Mkristo. Kama mama Muislam, baba itakuwa kinyume cha hapo.
ke waNaibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), January Yusuf Makamba.
TOFAUTI HATA KWA MKE, MUME
Maalim
Hassan akaenda mbele zaidi kwa kusema: “Kama wazazi wake wote watakuwa
dini moja, basi yeye (mgombea) atakuwa na imani tofauti na mke wake au
mume wake (kama kutakuwa na mgombea mwanamke). “Mgombea anaweza kuwa
Muislam, kama ni mwanaume basi mke wake atakuwa Muislam. Vivyo hivyo kwa
mgombea mwanamke,” alisema Maalim Hassan.
KWA HARAKAHARAKA
Kauli
ya Maalim Hassan ina ishara ya kumgusa moja kwa moja, Naibu Waziri wa
Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Bumbuli (CCM), January Yusuf Makamba ambaye mama yake mzazi ni Mkristo
huku baba yake, mzee Yusuf Makamba akiamini katika Uislam.
WANAOTAJWA KUWANIA URAIS MWAKA HUU
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitangaza nia hiyo usiku Agosti 22, mwaka jana Ikulu Ndogo ya Jiji la Mwanza.
Margreth Sita.
January
Makamba alitangaza nia ya kuwania nafasi hiyo Julai 2, mwaka jana
alipokuwa Uingereza katika mkutano wa sekta ya mawasiliano. Wengine ni
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Andrea Kigwangallah, Naibu Waziri wa
Fedha, Mwigulu Lameck Nchemba (CCM), Waziri Nyalandu (CCM), Mawaziri
Wakuu Wastaafu, Frederick Tuluwai Sumaye na Edward Ngoyai Lowassa (wote
CCM).
Wengine
ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camillus
Membe (CCM), Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Masatu Wassira na
Mbunge wa Sengerema, William Mganga Ngeleja (CCM). Waziri wa Uchukuzi,
Samuel John Sitta naye amekuwa akitajwa kujitosa kwenye kijiti cha
urais.
Kutoka
vyama vya upinzani, ambaye ameshatangazwa na chama chake ni Mwenyekiti
wa Cuf, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba. Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad
Peter Slaa yeye amekuwa akigombea kwa chama hicho kwa miaka kumi
iliyopita. Lakini kuna tetesi kuwa, huenda Chadema ikamsimisha
mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Haikaeli Mbowe.
-GPL