Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Mahusiano na Uratibu, Mary Nagu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Wiliam Lukuvi.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Steven Wassira.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amebadili mawazini na naibu mawaziri Ikulu leo.
Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao leo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi
ya Rais, Sifue Ombeni alitaja mawaziri hao wapya ambao wanaapishwa
jioni hii na wizara zao kwenye mabano kuwa George Simbachawene (Nishati
na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe,
(Afrika Mashariki).
Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira
(Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama
(Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu
Uwekezaji na Uwezeshaji).
Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama
ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah
Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna
Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati
na Madini).