Ticker

10/recent/ticker-posts

MSANII DRAKE AMEINGIA KWENYE KASHFA NYINGINE YA UGOMVI, ISOME STORI YAKE HAPA.

drake ii
Drake amekuwa moja ya mastaa ambao wamekuwa wakikaa kwenye headlines mara kwa mara kutokana na sababu mbali mbali.

Safari hii Drake ameangusha kitita kikubwa cha fedha wakati akiwa anaharakisha kuingia ndani ya club ambapo waliomuona wanasema jamaa alikuwa kama amekasirishwa na kitu hivi, kwa hiyo hata huko alikokuwa anaingia huenda hakukuwa na jambo la kheri.
Staa huyo alikuwa anasherehekea birthday yake wikiendi iliyopita Club Stadium, Washington D.C Marekani ambapo baadhi ya watu waliokuwa ndani ya club wanasema huenda Drake alikasirishwa na kitendo cha mmoja ya marafiki zake kupigwa na mtu asiyefahamika.
Drake III
Moja ya sababu ambazo huwa zinamuweka Drake kwenye headlines ni ugomvi, kwa hiyo kama aliingia kushiriki ugomvi wowote ndani ya club, bado si tukio geni kwa wale wanaomfahamu staa huyo.

Credit:Millardayo