Ticker

10/recent/ticker-posts

MSANII DUDUBAYA NAYE ATOA KAULI YAKE UGOMVI WA ALI KIBA NA DIAMOND..MSIKILIZE

Msanii DUDU BAYA
Dudubaya anajulikana kama mmoja wa Wasanii wa siku nyingi bongoflevani ambae pamoja na headlines zake binafsi huwa anasikika mara chache akizungumzia au kutoa ushauri kwa ishu kadhaa za Wasanii wenzake. Baada ya kusikia yanayoendelea kati ya mastaa wa bongofleva Diamond na Ally Kiba kwamba wako kwenye beef, Dudubaya alikutana na AyoTV Dar es salaam na kuyasema yafuatayo >> ‘Wasanii wa Tanzania tuna wapambe na sio marafiki kwa sababu mpambe unaweza kuwa umelewa yeye ndio anakoleza ugomvi lakini rafiki ni yule anaekuonya au kukushauri’

Ali Kiba alifanya ngoma na R.Kelly nikafurahia na nikapenda kinoma kupiga salute kwa mdogo wangu anakwenda next level, Diamond kaja kufanya vizuri na ninafurahia… muziki huu unakosa nguvu kwa sababu ya roho mbaya, wivu na chuki na kutokuwa makini na wanaotuzunguka, anakwenda kwa Diamond anasema hivi kisha anakwenda kwa Ally Kiba anasema hivi’ – Dudubaya ‘Ninachowashauri hawa wadogo zangu watulie chini wajitambue ni Wasanii na usanii wao ni wa kutengeneza pesa, tena watengeneze hata Tour ya Amani wazunguke nchi nzima.. wazunguke hata Afrika Mashariki na sio hizi beef’ ‘Siku moja nilikua na Dully Sykes na Christian Bella alafu watu wakawa wanasema Diamond ooohhh sijui kashindaje tuzo saba, nikawaambia hivi ukiwa na akili timamu wimbo kama ‘my number one’ kila kona unayopita, video mpaka TV za kimataifa zinapiga alafu leo unaweza video yako ya kijingajinga unategemea kuishinda ‘my number one’ …….Diamond alistahili kushinda hizo tuzo saba, mimi sikuona cha ajabu’ Kwenye sentensi nyingine Dudubaya amesema ‘kuna gazeti moja liliandika eti Diamond alihonga hela kuchukua hizo tuzo, ni vitu vya kipumbavu kabisa… hujui kusoma lakini picha lazima uione, Ali Kiba na Diamond kila mmoja ana mama yake, wakae chini kama binadamu wajitambue, waachane na mambo ya watoto wa hapa mjini hawa ni wapambe tu mwisho wa siku hawana msaada’ Unaweza kumsikiliza Dudubaya zaidi hapa kwa kubonyeza play kwenye rangi ya orange hapa chini.

Post a Comment

0 Comments