Simba Wamaliza Kazi iliyowapeleka Zanzibar, Al Ahly Hawatoboi Zindiko Limekubali

 Simba Wamaliza Kazi iliyowapeleka Zanzibar, Al Ahly Hawatoboi Zindiko Limekubali

Kikosi cha Simba SC kimeanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam kikitokea kisiwani Unguja, Zanzibar baada ya kumaliza kambi ya maandalizi ya Mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaowakutanisha dhidi ya Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Al Ahly kutoka nchini Misri, utakaopigwa Ijumaa (Machi 29) Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Simba SC wachezaji wa Simba SC wameonekana wakiwa bandarini kisiwani Unguja, tayari kwa safari ya kurejea Dar es salaam.

Hata hivyo Simba SC inatarajiwa kuendelea na maandalizi ya mchezo huo ikiwa jijini Dar es salaam, huku wapinzani wao wakitarajiwa kuwasili nchini kesho Jumatano (Machi 27).

Ikumbukwe kuwa Mshindi wa jumla wa mchezo huo atatinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na atakutana na Mshindi wa mchezo katia ya Petro Atletico (Angola) dhidi ya TP Mazembe (DR Congo).

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال