Waliomuua Dereva wa Watalii Karatu Wakamatwa


 Jeshi la Polisi limesema kifo cha Dereva wa Watalii, Omary Saimon Msamo kilichotokea Wilayani Karatu, Machi 16, 2024 kimetokana na kuuawa ambapo Anthony Paskali ‘Lulu’ na Emmanuel Godwin Joseph wakazi wa Karatu wanashikiliwa kwa mauaji hayo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime amesema “Waliohusika walilenga kumpora, Watuhumiwa wamekamatwa na wamekutwa na simu ya marehemu ila fedha walizompora Tsh 200,000 walikuwa wameshagawana na kuzitumia, walimpora baada ya kumpiga kisogoni na kudondoka chini.”

Awali, ilidaiwa kifo hicho kimetokana na Askari Polisi kumjeruhi Omary baada ya kukamatwa njiani akituhumiwa kuendesha gari akiwa ametumia kilevi. Misime amesema Jeshi la Polisi linatoa tahadhari juu ya kueneza taarifa za uongo, chuki na uzushi dhidi ya mtu mwingine au Taasisi.

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال