Ticker

10/recent/ticker-posts

Breaking Newz: Afisa wa Polisi Akamatwa na Misokoto 40 ya Bangi..Jionee hapa


Afisa mmoja wa Polisi nchini Kenya, Kobstabo Evans Otieno amesweka rumande katika Kaunti ya Makueni akidaiwa kushiriki maandamano, huku akiwa na misokoto 40 ya bangi yenye thamani ya Shilingi 2,000.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka huduma ya Polisi -NPS, Kobstabo Otieno alikamatwa eneo la Emali katika barabara kuu ya Nairobi kuelekea Mombasa na tayari amesimamishwa kazi akisubiri kusomewa shitaka linalomkabili.

“Tunathibitisha kukamatwa kwa afisa huyo kupitia tukio lililonakiliwa kwa nambari OB:15/20/7/2023 saa nne na dakika 20 mchana na alikamatwa alipokuwa akipanga waandamanaji katika kizuizi haramu cha barabarani,” taarifa ya Mkuu wa Polisi, Japhet Koome ilisema.

Aidha, ripoti hiyo imeeleza kuwa, “Afisa huyo alikuwa miongoni mwa raia waliokuwa wakihangaisha wenye magari kwa kuwavurumishia mawe. Aidha, imebainika kuwa afisa huyo alionekana na wenzake katika mji wa Emali akiwa miongoni mwa waandamanaji waliorusha mawe katika kituo cha polisi cha Emali.”

Post a Comment

0 Comments