Ticker

10/recent/ticker-posts

Mwigulu Nchemba Awakemea Wanasiasa Wanaoihusisha Serikali na Kushambuliwa kwa Tundu Lissu


Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kuumia kwa mbunge Tundu Lissu kama chambo ya kisiasa katika majukwaa.

Dkt. Mwigulu amesema hayo jana mkoani Singida wakati wa kampeni za udiwani kata ya Mitunduluni.

Mwigulu  amewataka wanasiasa  waache kutumia matatizo ya ndugu yao kama mitaji ya kisiasa badala  yake waje na hoja za maana za kusaidia katika maendeleo ya nchi.

Aliongeza kusema kuwa mwaka uliopita uhalifu wa ajabu ulitokea ambapo kuna watoto wadogo wa chekechea walitekwa na kuuwawa ambao hawakuwa  hata na  shida na mtu yoyote na wazazi wao ni watu wa kawaida kabisa je serikali ndio imehusika.

“Sisi tunaoshughulika na maswala ya uhalifu tunatafuta wahalifu wanaofanya maswala ya kihalifu, kuna watu wanaona ni ajenda ya kisiasa wakati sisi tunaombea mtu apone” alisema Dkt. Mwigulu

Dkt. Mwigulu ameongeza na kusema kuwa je angeamua kuendelea  kusema kuhusu kupigwa risasi kwa mwanajeshi masaki inauhusiano gani na shida za kata ya Mitundulini, hivyo wananchi wa Singida wawaadhibu kwa kuwanyima kura katika uchaguzi wa tarehe 17 mwezi huu.

Uchaguzi mdogo katika kata ya Mitunduluni unafanyika baada ya Diwani aleyekuwepo katika kata hiyo kufariki dunia kwa maradhi. VIDEO: