Ticker

10/recent/ticker-posts

Aina 5 za kuachana kwenye mahusiano (5 ways to breakup)


1. Kuchemka hadi kumwagika “The Boil Over”
Katika hali hii unaanza kuziona dalili za kuachana kwenu kwa mbali. Labda mwenzako amekuwa akifanya au kusema vitu fulani kwa muda mrefu na vimekuwa havikufurahishi, kila unapotaka kumpasukia kunakitu kinakwambia subiri, mpe nafasi nyingine, ndani yako unajiona kabisa kuwa wakati umewadia sasa wa kumpasha habari yake kwa mara ya kwanza na ya mwisho, na pia ndani yako unakuwa na utayari wa kubeba majukumu kwa chochote utakachomwambia. Gafla sikumoja kinatokea kitu kidogo tu, labda ni neno lililosemwa au kitu kilichofanywa na wewe au mpenzi wako, mnagombana na kutofautiana sana na kutokana na machungu na maumivu ya muda mrefu moyoni mmoja anaamua kuutumia upenyo huo kulitamka neno “it’s over” (naomba tuachane) na huo unakuwa mwisho wa penzi lenu.

2. Kuachana kimlipuko
Yako baadhi ya mahusiano ambayo huwa yana vipindi vya amani kwa kitambo kidogo na milipuko ya magomvi kwa kipindi kingine. Milipuko hii simaanishi kule kutoelewana kwa kawaida bali mahusiano yanakumbwa na milipuko ya kutoelewana kwa kitu fulani kizito, au ugomvi unakuwa mzito na wenye kuyumbisha pande zote mbili. Kwa mfano baada ya kitambo cha amani na mapenzi kunagundulika mahusiano ya pembeni kwa mmoja wa wapenzi na hili linazua mlipuko wa ugomvi ambao gafla unalizima penzi na ule ukaribu wenu unafifia ghafla na kutokomea jumla. Yamkini ni mlipuko mmoja tu umetokea lakini mpenzi mmoja aliyeumizwa hatamani hata kumwona mwenzake kwa macho, wapendanao hawa wanajeuka maadui ghafla utadhani hawakuwahi kupendana.

3. Leo nje kesho ndani, kesho baridi kesho kutwa moto
Hii ni staili ya kuachana ambayo wengi wetu huitumia mara kwa mara na maranyingine pasipo mhusika mmoja katika penzi kufahamu kwamba safari ya kuachana ndiyo inawadia. Katika mahusiano ya watu wa namna hii kunakuwa na mazingira yanayowafanya leo wanakorofishana kesho wanapatana, kesho wanakuwa pamoja keshokutwa unaskia hawapo tena pamoja, mara unasikia wamerudiana, tena wanakuja kufarakana na tabia hii inakuwa ndiyo maisha yao ya kilasiku na mfumo wa mahusiano yao. Tabia hii huendelea kudumu hadi inafika nyakati mmoja akitoka basi anatoka jumla, kila mwenzake akiwaza kwamba yamkini atarudi kama mazoea yao yalivyo lakini haiwi hivyo tena na penzi lao linakatikia hapo.

4. Mkate ulioungua “The burning bread”
Mara nyingi tunapopika mkate huuweka kwenye joto kali ili uive na mara kwa mara muokaji huuangalia kama umeiva kwa kuutumbukizia kitu kikali kama vile uma ili kuangalia hali yake ya ndani ilivyo na kufahamu maendeleo ya uivaji wake. Mkate uliosahaulika kuangaliwa mara kwa mara huungua na muokaji anapokuja kuutoboa ndipo anapofahamu kuwa mambo yameshaharibika na mkate sio wakuliwa tena.

Katika mahusiano yetu hususani kwa baadhi ya wale walioweza kukaa muda mrefu au hata waliooana, bahati mbaya kwasababu ya masumbufu ya maisha ya kilasiku na mapenzi ya kimazoea wakasahau kuchochea na kuziamsha hamasa za penzi lao kila mara, hisia za ukaribu ndani yao kufa, penzi hilo taratibu huonekana kushuka na kupoa na taratibu pasipo wapendanao hawa kugundua kilakitu kinakuwa cha baridi, kisicho na ladha na kilammoja akitamani penzi jipya la tofauti na yamkini kutoka kwa mtu watofauti sio huyu tena. Hii inapelekea wawili hawa kuchagua kuachana, tena mara nyingine kwa mmoja kugundua kuwa mwenzake anampenzi mwingine.

5. Ghafla moto ghafla kupoa “Microwave style”
Kama umewahi kutumia mashine ya kupashia joto chakula “microwave” utaelewa kitu ninachojaribu kuzungumza hapa. Yako mapenzi ambayo yameanzishwa gafla sana na yaka paa juu sana, kila mmoja akimhisi mwenzake kiukaribu sana, na hisia za wawili hawa zinakuwa za moto kama zilizowekwa kwenye ‘microwav’e, kila mmoja akihisi kwanini hatukujuana awali, kwasababu ni kama vile Mungu alituumba tuwe pamoja kuanzia tukiwa wadogo, lakini ghafla mmoja kati ya wapendanao hawa anazimika na kutoendeleza tena moto uliokuwepo. Kwa mfano mlianza ghafla kuhusiana na mapenzi yakawa moto kuliko mlivyofikiri, kilasiku mkowote na lazima muonane, ghafla mwenzako hapokei simu, na wala akiiona simu yako hawajibiki kukupigia, na tabia hiyo inaendelea hivyohivyo hadi unakata tamaa na unaamua kukubali yaishe. Mapenzi haya yaliwaka na kuzima kwa mtindo wa microwave. Mara nyingi wapaenzi wanaoachana kwa aina hii ni wale waliokutana kwenye mazingira kama vile safarini, kwenye basi, treni au ndege, waliokutana kwenye muziki au sherehe nk.