Ticker

10/recent/ticker-posts

HEBU ANGALIA WEMA SEPETU NA PENNY WAKIMKEJELI DIAMOND NA ZARI THE LADY BOSS

Stori: Imelda Mtema Mastaa wawili hapa Bongo ambao huko nyuma walikuwa katika bifu kali, Wema Sepetu na Penny Mwingilwa wameonekana kumkejeli aliyekuwa mpenzi wao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kutumia neno Project.
Mastaa hao walionekana wameweka picha yao wakiwa pamoja wamejilaza chini nyumbani kwa Wema  na kuandika kuwa wakiwa katika Project yao neno ambalo lilitumiwa na Diamond akiwa na mwanadada Zarina Hassan  ‘Boss lady’ anayedaiwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki huyo.
Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na Penny kwa njia ya simu ambapo alisema kuwa siku hiyo walikutana na kuzungumza na rafiki yake huyo wa muda mrefu na mambo ya project yalitokea tu. “Sisi tulimisiana sana na tulikutana na kuzungumza mambo mengi ya zamani, hiyo project iliingia tu,” alisema Penny. GPL