Kennedy Musonda wa Yanga Aifunga Ivory Coast na kuipeleka Zambia AFCON 2025

 Kennedy Musonda Atupia na Kuipeleka Chipolopolo AFCON 2025

Timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ imefuzu kwenda AFCON 2025 baada ya kuwalaza Mabingwa watetezi, Ivory Coast kwenye mchezo wa raundi ya 5 wa kufuzu michuano hiyo itakayofanyika Nchini Morocco.

Bao pekee la Kennedy Musonda limewapeleka Chipolopolo kileleni mwa Kundi G wakifikisha pointi 10 baada ya mechi 5 huku Ivory Coast wakiporomoka mpaka nafasi ya pili wakiwa na pointi 9.

Sierra Leone wanakamata nafasi ya tatu wakiwa na pointi 5 huku Chad wakiburuza mkia wakiwa na pointi tatu.

FT: Zambia 🇿🇲 1-0 🇨🇮 Ivory Coast

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال