Mwigizaji Mkongwe wa Nigeria Amaechi Muonagor Afariki Dunia

 Mwigizaji Mkongwe wa Nigeria Amaechi Muonagor Afariki Dunia

Mwigizaji Mkongwe wa Nollywood Nigeria Amaechi Muonagor (62) amefariki baada ya kuugua magonjwa mbalimbali huku kufeli kwa figo yake kukitajwa pia kama sehemu ya chanzo cha kifo chake.

Ripoti za kifo chake zimegusa hisia za Watu wengi hasa kutokana na video yake kusambaa hivi karibuni akiomba Watu wamchangie ili asafiri nje ya Nigeria kwa ajili ya matibabu ambapo tayari Watu mbalimbali wa ndani na nje ya Nigeria walianza kumchangia.

Kifo cha Amaechi kinakuja wiki chache tangu kilipotokea kifo cha Legend mwingine wa Nollywood Mr. Ibu ambaye alifariki March 02,2024 akiwa anapatiwa matibabu Jijini Lagos, Nigeria.

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال