Ticker

10/recent/ticker-posts

Soma Historia ya Lowassa:Mwanzo na mwisho wa Safari ya matumaini ndio huu

Anaandika kijana Mzalendo  na Mchapakazi Gibson George Bayona (pichani)kutokea Monduli Mkoani Arusha ambapo mazishi ya Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Ngoyai Lowassa yatafanyika kesho 17/02/2024 kijijini kwao Ngarashi Wilayani Monduli Mkoani Arusha.Soma makala hii ujifunze👇👇👇

*MWANZO NA MWISHO WA SAFARI YA MATUMAINI*

Na Gibson George Bayona

Tafakuri nikiwa njiani kuelekea MONDULI;

“Mamia ya marafiki wa Edward Lowassa waliokuwa wanaamini katika SAFARI YA MATUMAINI iliyojengwa katika ndoto za Urais wa Tanzania za Edward Lowassa walikua wakisafiri kila mwisho wa mwaka kwenda Monduli, kwa ajili ya kula pamoja, kukesha na kutafakari pamoja juu ya ndoto hiyo iliyodumu kwa miongo miwili.

Tangu  Lowassa alipojiuzulu  wadhifa wa uwaziri mkuu Februari 2008 na kuanza rasmi kujipanga kwa ajili ya kukielekea kiti cha Urais 2015, wapo maelfu ya watu waliofika Mondoli katika sherehe maalum za kufunga mwaka zilizokua zikifanyika huku mamia ya ng’ombe na mbuzi, kuchomwa na kuliwa ili tafakuri kuhusu safari ya matumaini iweze kwenda vizuri.

Picha halisi ya leo Viongozi wa Kitaifa, Chama na marafiki ndugu na jamaa wakila Nyama choma ndio ulikua utaratibu wa makutano ya wadau wa SAFARI YA MATUMAINI kipindi hicho, na hii ndio tafasiri halisi ya mwanzo na mwisho wa Safari hii ambayo itatamatishwa rasmi kesho ENL atakapolala kwenye nyumba yake ya Milele.

“Tulifurahi pamoja, tukahuzunika pamoja na tutashinda pamoja”, hii ndiyo kauli mbiu iliyowaunganisha wana mtandao walioamini katika SAFARI YA MATUMAINI. Hawakuchoka kusafiri mara kwa mara kwenda Monduli, huku idadi ya wanaoamini katika safari hii wakiziki kuongezeka kila mwaka na wanaosafiri kwenda Monduli wakiongezeka pia.

Miaka takribani 8 na nusu tangu SAFARI YA MATUMAINI ishindwe kutimia mnamo mwaka 2015, sasa Watanzania walioamini katika safari hiyo na wale ambao hawakuamini sote kwa pamoja tunaungana kumsindikiza Edward Ngoyai Lowassa katika SAFARI YAKE YA MWISHO, ambayo matumaini yetu ni kwamba TUTAONANA TENA na mpendwa wetu huyu.

Wingi wa watu wanaoenda Monduli katika SAFARI YAKE YA MWISHO unaendelea kuonesha jinsi ambavyo Lowassa alijenga ushawishi mkubwa katika akili na mioyo ya watu. Hakuchoka kuiota na kuipigania ndoto yake kuu huku ikikolea na kukomaa kadri miaka inavyokimbia.

Viongozi vijana tukijiandaa kumpumzisha Lowassa katika nyumba yake ya milele na tutakapokua tunakula ng’ombe zaidi ya 200 waliotolewa na viongozi wa kimasai ili wachinjwe kuliwa na waombolezaji basi tule nyama hizo huku tukitafakari juu ya kutochoka kuzipigania ndoto zetu bila kujali nyakati ngumu tunazopita.

Maelfu ya marafiki wa Lowassa walioshiriki kusafiri naye katika SAFARI YAKE YA MATUMAINI wanatukumbusha sisi vijana kuhusu umuhimu wa kutengeneza mtaji wa marafiki wengi wa dhati wa kusafiri nao katika ndoto zetu.”

Post a Comment

0 Comments