Ticker

10/recent/ticker-posts

Watanzania Wacharuka ishu ya Staa Rick Ross Kupanda Mlima Kilimanjaro

Rapa wa Marekani, William Roberts II 'Rick Ross' ameeleza kuwa anajifua kuja kupanda Mlima Kilimanjaro, Januari mwakani, suala lililowaibua Watanzania mitandaoni kuhusiana na mlima huo.

Ross aliweka video mtandaoni akifanya mazoezi kujiandaa kupanda mpaka kileleni mwa mlima huo na kisha mtandao rasmi wa Rap kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ukaweka taarifa hiyo bila ya kueleza mlima huo unapatikana nchi gani.

Hilo lilifanya Watanzania 'kuvamia' ukurasa wa mtandao huo na kufafanua kuwa mlima huo upo Tanzania ikiwemo kuweka alama ya bendera ya Tanzania na wengine wakimkaribisha rapa huyo aliyewahi kushirikishwa na Diamond Platnumz kwenye Wimbo wa Waka waka uliotoka mwaka 2017.

Jack the Giant aliandika: "Mlima Kilimanjaro upo Tanzania, Mkoa wa Kilimanjaro, karibu Tanzania Rick Ross." Naye Gerrard Smith alihoji: "Kusema (mlima) upo Tanzania hamuwezi sio?"

Mbali na hayo, maoni mengine yalikuwa ni ya kujivunia na kufurahia kwa Ross kuhitaji kupanda mlima huo wenye urefu wa meta 5,895 kutoka usawa wa bahari.

Aidha, mwaka jana Ross aliwahi kutoa ahadi ya kupanda mlima huo uliofunikwa na theluji alipokuwa akihojiwa na Full Send Podcast ikiwa pia ni miongoni mwa majaribio magumu anayopanga kuyafanya kila mwaka kwa ajili ya mashabiki wake.

Post a Comment

0 Comments