Ticker

10/recent/ticker-posts

Mchambuzi Shaffih Dauda asema "Kocha Robertinho Hakupashwa Kufukuzwa na Simba"

 

Mara nyingi naamini matokeo bora ya timu ni mchanganyiko wa uwajibikaji wa wahusika wote kuanzia bodi ,menejimenti ,benchi la ufundi ,wachezaji na wengine mfano mashabiki

Mfano kutoka kwa kiongozi wa juu kuja chini ukaangalia mfumo je upo sawa ? Rais wa heshima ana mchango gani ? anakutana na bodi wakati gani ? bodi ifanye nini ? hivyo hivyo kuja chini hadi kwa watu walio nje

Juzi Rais wa heshima alisajili timu nyingine ya watu ambao ni nje ya timu

Uongozi ulioshinda na kuingia madarakani sidhani kama ulikuwa unapata sapoti

Ni vitu vingi ambavyo kwa jicho la kawaida havionekani lakini vina mchango mkubwa sana, football ni team game not an individual game ( mpira ni mchezo unaohusisha timu / umoja na sio mtu mmoja mmoja

Mkishinda mnashinda wote na mnafungwa wote mfano zoezi la kuvaa medali linakupa picha halisi ya kuona kuna wakina nani nyuma ya wachezaji kama timu

Mimi kama Dauda siamini kama Robertinho anatakiwa kufukuzwa ,ukija head to head Robertinho na Yanga kashinda mechi moja ,sare mechi moja na kafungwa mechi moja na hiyo sare bado alipata ubingwa (ngao)

Inawezekana kuna sababu zingine ambazo hawawezi kuzitaja ,ndio maana taarifa inasema makubaliano ya pande mbili

Post a Comment

0 Comments