Ticker

10/recent/ticker-posts

Mbunge Babu Tale kumdhamini Mtoto Mwenye Kipaji Aliotrend Mtandaoni, Kuimba Wasafi Festival na Kurekodiwa Bure

 Babu Tale Ampa Shavu Dogo Mwenye Kipaji Aliotrend Mtandaoni, Kuimba Wasafi Festival na Kurekodiwa Bure

Meneja wa supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye ni Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Taletale 'Babutale' amemfungulia njia kijana mwenye kipaji 'Founder TZ' ambaye ameonyesha uwezo wake mkubwa wa kuimba kupitia mitandao ya kijamii

Mdau huyo mkubwa wa muziki ameshare video ya msanii huyo na kuandika; “Nimependa huyu dogo anavyoimba na kwakua tumeumbwa kuwainua wenzetu basi kwenye hii Wasafi Festiva.

"Pia ningependa kuona hi nyota ikiendelea kuwaka. Haya kwa anayemfaham huyu kilana aniletee kwene ofisi za wasafi. Nataka nimpe ofa ya Video na audio ili atimize ndoto zake. #theblackgodfather,” amesema Tale.

Kauli hiyo ni kama sheria na njia, kwani mdau huyo mkubwa wa muziki nchini Tanzania amewahi kufanya hivyo kwa wasanii wengi wachanga wa nje ya WCB na wakatoboa

Post a Comment

0 Comments