Ticker

10/recent/ticker-posts

Waziri Mavunde:Tunajenga Mradi mkubwa Mto Ruvuma,Ruhuhu na Litumbandyosi,asema ni Maelekezo ya Rais Samia

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde 
Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan imetenga fedha katika bajeti ya mwaka 2023/24 kwa ajili ya utekelezaji mkubwa wa miradi ya umwagiliaji katika bonde la Mto Ruvuma,Ruhuhu na Litumbandyosi yaliyopo mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mh.Dkt. Philip Isdor Mpango katika Wilaya za Nyasa na Mbinga,Mkoani Ruvuma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango

Akizungumza na wananchi wa wilaya za Mbinga na Nyasa,Makamu wa Rais Dkt. Mpango aliwapongeza wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kwa mchango wao mkubwa kwenye usalama wa chakula hapa nchini kutokana na uzalishaji mkubwa wa mazao ya nafaka hasa mahindi na kutumia fursa hiyo kuitaka Wizara ya Kilimo ieleze jinsi ilivyojipanga katika utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji.

Akitoa maelezo ya Wizara ya Kilimo Naibu Waziri Mavunde alieleza yafuatayo;

-Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya umwagiliaji mkoani Ruvuma ili kuongeza uzalishaji wa mazao.

-Kwa mwaka wa fedha 2023/24 Serikali itafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na ujenzi wa miumbombinu ya Umwagiliaji katika Bonde la Mto Ruvuma lenye jumla ya hekta 26,066,Mto Ruhuhu lenye hekta 3,700 na Litumbandyosi hekta 900 pamoja na uchimbaji wa mabwawa makubwa matano(5) na ukarabati wa skimu za umwagiliaji  katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Ruvuma.

-Mkoa wa Ruvuma wamezalisha zaidi ya tani milioni 1 ya mahindi,ni mkoa ambao serikali itawekeza kiasi kikubwa kwenye kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao.

-Serikali itaendelea kusimamia upatikanaji wa soko la uhakika la mazao ya wakulima,na kwasasa Wakala wa Hifadhi ya Chakula(NFRA) wamefungua vituo 17 vya ununuzi wa Mahindi katika wilaya za Mkoa wa Ruvuma.

-Mbolea za Ruzuku zitaendelea kutolewa kama msimu uliopita,na kwasasa tumesajili vituo vingi zaidi vya mauzo ya mbolea ili wakulima wasiifute mbolea umbali mrefu kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Post a Comment

0 Comments