Ticker

10/recent/ticker-posts

SIMANZI: Mwanafunzi wa Chuo Ajinyonga Hadi Kufa, Kisa Hiki hapa...Aandika Haya Whats App Status

Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) Mkoani Mtwara aliyetambulika kwa jina moja la Regan ambaye amekuwa akiishi Mtaa wa Chikongola, Manispaa ya Mtwara- Mikindani anadaiwa kujinyonga hadi kufariki na mwili wake kukutwa ndani ya chumba chake.


Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa jana July 4,2023 majira ya saa sita mchana na hadi sasa sababu zilizofanya ajitoe uhai hazijajulikana.

Baadhi ya Mashuhuda wameeleza hisia zao na kusema huenda Kijana huyo aliamua kujitoa uhai kutokana na masuala ya kimapenzi kwasababu Siku sio nyingi alikua amegombana na Mpenzi wake waliyekuwa wakiishi pamoja.

Kamanda wa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema amepokea taarifa za tukio hilo na atalitolea ufafanuzi baada ya uchunguzi wa Madaktari kukamilika na kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Ligula.

Marehemu Reagan muda mfupi kabla ya kujitoa uhai aliweka picha yake ya utoto kwenye WhatsApp Status yake na kuandika maneno yafuatayo ——> “🙏🏾 kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa, maana WEWE NI MAVUMBI NA MAVUMBINI UTARUDI”

Post a Comment

0 Comments