Ticker

10/recent/ticker-posts

Mifuko ya Plastiki yapigwa marufuku Hospitali ya Taifa Muhimbili

 

Mifuko ya Plastiki marufuku Muhimbili
UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili umepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwa watoa huduma na ndugu wa wagonjwa katika mazingira ya hospitali (Upanga na Mloganzila), ikiwemo wodini na maeneo mbalimbali ya kutolea huduma.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma (MNH), Aminiel Aligaesha katazo hilo linatolewa kufuatia uwepo wa mifuko ya plastiki kwenye mazingira ya hospitali iliyopigwa marufuku na serikali nchini.

“Mifuko hii inaletwa na baadhi ya ndugu wa wagonjwa ambao huitumia kama vibebeo vya chakula wanapokuja kutembelea ndugu zao waliolazwa wodini na baadhi ya watoa huduma hospitalini hapa,” amesema Aligaesha.

Amesema kuwa katazo hilo linaanza mara moja na ni kwa kampasi zote mbili za Hospitali ya Taifa Muhimbili ambazo ni Upanga na Mloganzila.

______

Post a Comment

0 Comments