Ticker

10/recent/ticker-posts

Spika Dkt Tulia atoa msaada wa Milioni 100 Kwa Wanawake wa Mbeya

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amewawezesha wanawake 1000 jumla ya shilingi 100,000,000 kutoka Halmashauri saba za Mkoa wa Mbeya.

Hafla ya kukabidhi fedha hizo imefanyika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya na kuhudhuriwa na viongozi mbaimbali wa Chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Beno Malisa aliyemuwakilisa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa Dkt. Tulia Ackson kutoa fedha kwa wanawake wajasisiamali ambapo mwaka wa kwanza aliwawzesha wanawake 400 mwaka jana aliwawezesha zaidi ya wanawake 600 na mwaka huu wanawake 1000 na kufanya jumla ya wanawake 2000 kunufaika na misaada hiyo.

Awali Dkt. Tulia aliwaambia wananchi kuwa amedhamiria kubadilisha maisha yao kwa nguvu zake zote ili kutengeneza historia ambayo haijawahi kutokea katika Mkoa huo ikiwemo kuyagusa maeneo mbalimbali.

“Mungu akituwezesha mwakani tutaongeza idadi na si hawa waliopata leo, tumekuwa tukizigusa kila sekta na tutaendelea kuhakikisha tunaboresha maisha ya kila mwananchi wa Mbeya” alisema Dkt. Tulia

Mwenyekiti wa Bajaji Festo Mwasimba amemshukuru Dkt. Tulia Ackson kwa namna ambavyo siku zote anahangaika kuhakikisha anawakwamua kiuchumi wananchi wake bila kujali nafasi zao za kidini, chama n.k

Aidha Aliko Fwanda Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji la Mbeya amesema tangu Dkt. Tulia achaguliwe kuwa Mbunge vijana wengi wamejiajiri na kumiliki pikipiki zao hivyo kama vijana hawatakubali kumpoteza kwa namna yoyoye ile.


Post a Comment

0 Comments