Ticker

10/recent/ticker-posts

MJASIRI HAACHI ASILI:SHUHUDIA HAPA CHONGOLO AKILISHA MIFUGO NYUMBANI KWA BALOZI WA SHINA

Picha ikimwonyesha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo ambapo ameshiriki zoezi la kulisha mifugo nyumbani kwa mwenyekiti wa shina namba 4  Ndg. Martin Jackob Sangha  tawi la Simhha kata ya Hyderer wilayani Mbulu mkoa wa Manyara.

Katibu Mkuu ameshiriki zoezi hilo  tarehe 06 Machi 2023, ikiwa na lengo la kuhamasisha viongozi wote nchi nzima kuiga mfano wa balozi huyo kwa kuwa na shughuli rasmi ya ufugaji ambayo inamuingizia kipato halali na hategemei uongozi alionao ili kuishi.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Manyara akiambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Sofia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizeshani kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuhamasisha Uhai wa chama pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.


 

Post a Comment

0 Comments