Ticker

10/recent/ticker-posts

CHONGOLO,MJEMA NA USSI WATIKISA MOROGORO..JIONEE HAPA WAKIWA NA WANANCHI


Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo, akiwa pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi (Gavu) na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi, Ndugu Sophia Mjema, wakati msafara wake uliposimama eneo la Kinole, ukiwa njiani kwenda Kata ya Tegetelo, kukagua Mradi wa Maji wa Morong’anya. 

Akiwa hapo Kinole, mbali ya kuzungumza na kuwasalimia wananchi, Ndugu Chongolo aliwaongoza wajumbe wenzake hao wa Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ambapo moja ya mambo ambayo yamewafurahisha wananchi ni kuona katibu mkuu huyo ameshiuriki chakula cha mchana pamoja na wananchi hao wengi wao wakibaki wakisahangaa bila kuamini kwani wamesema walijua kwa ajili ya nafasi yake walishazoea viongozi wengi hawashiriki  chakula katika mazingira ya watu wa kawaida na kusema Chongolo ameonyesha uhalisia wa kuwa kiongozi asiye na makuu,mchapakazi na mwenye kujali.

Pia katika tukio hilo katibu wa itikadi na uenezi Ndugu Sophia Mjema alisimama na kuingia jikoni kuwasaidia wakina mama waliokuwa katika kazi yao ya kupika kisha kuwasaidia kusonga ugali na kusema alikosa nafasi ya kushiriki jambo kama hilo tangu muda mrefu lakini sasa ameingia katika utumishi wa chama hivyo kwake ni furaha kupika na kuwasaidia mama lishe hao huku akisisitiza yeye ni kiongozi hivyo hana budi kuonyesha ushiriki wake katika shughuli za kijamii. 


Post a Comment

0 Comments