Ticker

10/recent/ticker-posts

JIONEE JINSI BILIONI 215.6 ZA DMDP CHINI YA TARURA ZIILIVYOFANYA MAKUBWA KINONDONI

Adha ya mafuriko kwa wakazi wa Manispaa ya Kinondoni na Ubungo Jijinoi Dar es Salaam sasa imebaki kuwa historia baada ya jumla ya Sh bilioni 215.9 kutumika kujenga mifereji, mito na barabara za zege na lami kupitia Mradi wa Uendezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP) unaotekelezwa na TAURA.

 

Pia fedha hizo zimetumika katika usimikaji wa taa za barabarani zinazotumia nguvu ya jua, ujenzi wa njia za watembea kwa miguu, vyoo vya umma, masoko na sehemu za kupumzika katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Kinondoni na Ubungo.
 
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Mradi huo katika Manispaa ya Kinondoni, Mkelewe Tungaraza wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.
 
 

Alisema lengo kuu la mradi wa DMDP ni kuiwezesha serikali kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na kuibua fursa muhimu za uwekezaji ambazo hazijatumika ili kuboresha ukuaji na ustawi wa jiji la Dar es Salaam katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kujenga mwitikio wa dharura wa kukabiliana na majanga mbalimbali na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
 

Alisema jumla ya barabara za lami/zege zilizojengwa na kukamilika ni Km 70.21, ujenzi wa Mto Sinza wenye urefu wa Km 8.50, mfereji Kiboko Km 2.35, taa za Solar zilizosimikwa maeneo mbalimbali ni 1,939, mifereji mikubwa ya maji ya mvua Km 28.93, maeneo ya kupumzikia mawili, vyoo vya umma vitatu, Ofisi na Maabara, vyote vikiwa na vifaa.
 

Alitaja baadhi ya barabara zimejengwa katika maeneo ya Sokoni Makumbusho, Makanya- Tandale, Kisiwani – Kilimani, Simu 2000- Makumbusho, Kilongawima- Kyungi. External, Kisukuru, Majichumvi- Kilungule, Kilungule -Korogwe.

Wakizungumzia miradi hiyo, hususani ujenzi wa mifereji na mto Sinzani, Hussein Idrisa ambaye ni mkazi wa Sinza Mugabe alisema hapo awali hali ilikuwa mbaya kutokana na mafuriko lakini sasa wanalala kwa amani hata mvua ikinyesha.
 
Kauli hiyo iliungwa mkono na Christopher Mwakatuma ambaye aliishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kurekebisha miundombinu hiyo.


Post a Comment

0 Comments