Ticker

10/recent/ticker-posts

RC SENYAMULE AMWOMBEA BARAKA RAIS SAMIA KWA WAZEE WA DODOMA..." NAO WATOA TAMKO LAO HILI"

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameongoza kikao chake na wazee wa Mkoa wa Dodoma kilichofanyika wiki hii katika ukumbi wa Chuo cha Mipango  jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya Kumalizika kwa Kikao hicho ambacho moja ya mambo aliyoyaongelea ni Mikakati yake ya kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unainuka katika suala la elimu na hasa kwa kuhakikisha waalimu wakuu wa shule za Sekondari na Msingi wanatoa ripoti ya wanafunzi ambao kila wiki wanakuwa watoro kwani ni moja ya njia ya kudhibiti tatizo hilo.

Pamoja na Mengine Mhe.Senyamule amesisitiza umuhimu mkubwa wa wananchi kuheshimu Viongozi wa serikali wakiwepo wa ngazi zote pamoja na Mhe Rais huku wakimwombea Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwani anafanya kazi kubwa sana ya kuliongoza Taifa letu la Tanzania ili azidi kusonga mbele na kutovunjwa moyo na baadhi ya watu wasioona kazi kubwa anayoifanya.


Post a Comment

0 Comments