Ticker

10/recent/ticker-posts

SOMA HII TAARIFA MUHIMU TOKA OFISI YA KATIBU MKUU WA CCM MHE.DANIEL CHONGOLO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo atakuwa na Ziara ya Kikazi Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Katavi na Tabora akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Ziara hiyo itaanza Tarehe 13 - 24 Novemba, 2021 Mkoani Kagera katika Wilaya zote za Mkoa huo, na kuendelea katika Mikoa ya Geita, Kigoma, Katavi, na kuhitimisha mkoa wa Tabora.

Malengo ya ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Chama katika ngazi za Mashina pamoja na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025, ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa cha  tarehe 29 Juni, 2021.

Wajumbe wa Sekretarieti watakaojumuika katika Ziara na Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara Ndg. Christina Mndeme, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg. Kennan Kihongosi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Dkt. Philis Nyimbi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Ndg. Gilbert Kalima.

 

Post a Comment

0 Comments