Ticker

10/recent/ticker-posts

Rais Mstaafu Kikwete azungumzia saa za mwisho za Mkapa “nilimuona jana Hospitali, nimeshtuka sana” (+video)

Rais wa awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ametoa pole kwa Mama Anna Mkapa, Mke wa Rais Mkapa ambaye amefariki duniani usiku wa kuamikia leo.

Akizungumza baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Rais Kikwete amesema  kifo ni  siri ya Mwenyezi  Mungu, “ jana nilikwenda kumuona hospitali, tulizungumza sana, alikuwa na maumivu lakini ya kawaida, sio yale ambayo unaweza kusema nimemuona mgonjwa lakini…tulizungumza mengi.

“Nilipopata taarifa niliuliza kimetokea nini tena, kwa sababu hakuwa mgonjwa ambaye unaweza kutia shaka, niliondoka nikamuaga bwana nitakuja kukuona tena kesho, ila sikuombei uendelee kukaa  hospitali, natamani nije nikusalimie nyumbani, akaniambia naona nipo vizuri” Jakaya Kikwete Rais Mstaafu