Ticker

10/recent/ticker-posts

Mbunge Chadema Awakingia Kifua Wanafunzi Wajawazito

Mbunge Chadema Awakingia Kifua Wanafunzi Wajawazito

Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA Mkoa wa Geita, Upendo Peneza ameonesha kutofautiana na baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa huo, kwenye adhabu ya mtoto wa kike kufungwa jela iwapo atabainika kuwa ana ujauzito.

  kufuatia Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Boniphace Kazuzu kusema kuwa ni vyema mwanaume na msichana aliyepatiwa ujauzito wakatumikia kifungo cha jela wote kwa pamoja, ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano.

Peneza amesema adhabu hiyo itakuwa kali ukilinganisha na adhabu aliyonayo ya kuachishwa masomo ambapo kauli hiyo imeungwa mkono na Afisa Elimu wa Mkoa huo, Shabani Kamchacho akisema kuwa anahofu ya kuchukua hatua hiyo kwani jambo hilo linakwenda na masuala ya kisheria.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Hamimu Gwiyama ameeleza kusikitishwa na baadhi ya halmashauri mkoani humo kuficha takwimu sahihi za watoto wa kike kuachishwa  masomo kwa ujauzito.

Akifunga kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema upande wa makusanyo ya ndani kwenye halmashauri bado kuna changamoto,  hivyo amehimiza uwajibikaji kwa wahusika, huku mbunge wa geita Joseph Musukuma akichangia katika hilo.


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2SYEFv7
via

Post a Comment

0 Comments