Ticker

10/recent/ticker-posts

Hatimaye Halima Mdee Aachiwa kwa Dhamama

Hatimaye Halima Mdee Aachiwa kwa Dhamama
Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema),  jana Jumapili Februari 24, 2019 saa 10 jioni alipata dhamana baada kushikiliwa kituo cha polisi Oysterbay kwa zaidi ya saa 24.

Mdee  alikuwa akishikiliwa kituoni hapo baada ya kuitikia wito wa mkuu wa upelelezi mkoa wa kipolisi Kinondoni (RCO) Jumamosi Februari 23, 2019.

Hekima Mwasipu ambaye ni wakili wa Mdee amesema;"Tumehangaika tangu juzi lakini tunashukuru jana amepata dhamana ya polisi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili na kutakiwa kuripoti kwa mkuu wa upelelezi Februari 26”

Halima Mdee alidhaminiwa na Hekima na mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Anatropia Theonest.

Mdee anadaiwa kutoa kauli ya uchochezi alipokuwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Mikocheni, tarehe 21 Februari 2019.

from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2E9Agvf
via

Post a Comment

0 Comments